Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya kuruka viunzi Ban ataka serikali mpya Iraq iundwe

Baada ya kuruka viunzi Ban ataka serikali mpya Iraq iundwe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua kubwa ya kusonga mbele iliyofikiwa baada ya miaezi kadhaa ya kukwamba kuunda serikali mpya ya Iraq na amewataka viongozi wan chi hiyo kukamilisha mchakato kwa amani.

Katika taarifa yake Ban amesema anavipongeza vyama vyote vya kisiasa na viongozi wao kwa kufikia muafaka ambao utazingatia matakwa ya watu wote wa Iraq . Amewataka viongozi hao kuendelea kuonyesha moyo wa mshikamano katika kukamilisha mchakato huo na hatimaye kuundwa serikali mpya.

Ban ameyaatia maafikiano hayo baada ya kukwama kwa miezi minane kuwa ni hatua kubwa katika mchakato wa kuelekea demokrasia nchini Iraq.Amempongeza Rais Jalal Talabani kwa kuchaguliwa tena na kukaribisha uchaguzi wa spika wa baraza la wawakilishi na uteuzi wa waziri mkuu Nuri al-Maliki.

Baraza la usalama limekaribisha matokeo ya mchakato huo wa kisiasa uliojumuisha pande zote na kuwataka Wairaq sasa kujielekeza kwenye maridhiano ya kitaifa.Majadiliano ya kuundwa kwa serikali nchini Iraq yamekuwa yakiendelea tangu kufanyika kwa uchaguzi wa bunge mwezi Machi mwaka huu.