Skip to main content

Wafungwa wengine wa kisiasa waachiliwe pia Myanamar:Pillay

Wafungwa wengine wa kisiasa waachiliwe pia Myanamar:Pillay

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekaribisha kuachuachili Jumamosi jioni Aung San Suu Kyi katika siku ya mwisho ya kifungo chake cha nyumbani.

Bi Pillay ameitaka serikali ya Myanmar kuwaachilia pia wafungwa wengine 2200 wa kisiasa ambao bado wanashikiliwa nchini humo. Amesema hii ni ishara nzuri kwamba utawala wa Myanmar uko tayari kusonga mbele na changamoto kubwa za kidemokrasia na haja ya kuwa na maridhiano ya kitaifa.

Ameongeza kuwa kimsingi na dhahiri kwamba Aung San Suu Kyi anaweza kutoa mchango mkubwa katika mchakato huo. Pillay amesema ni muhimu kwamba kuachiliwa kwake si kwa vikwazo n kwamba hili linathaminiwa na kuenziwa kwa vitendo.

Hata hivyo kitendo cha kushikiliwa kwake kwa muda mrefu na kunyikwa haki bado ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kwa upande wa serikali ya Myanmar.Ameitaka serikali hiyo sasa kuwaachilia huru

wafungwa wengine wa kisiasa 2200, kama ishara kamili kwamba serikali hiyo mpya ina nia ya kuheshimu haki za binadamu na kuwa na mtazamo mpya wa siku za usoni kwa taifa hilo.

Pia amesema amesikitishwa kwamba Suu Kyi hakuachiliwa kabla ya uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa imetakiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na wengine wengi wakiwemo wajumbe wa ASEAN.