Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya zaidi ya muongo kizuizini Aung San Suu Kyi aachiliwa huru, Ban akaribisha hatua hiyo

Baada ya zaidi ya muongo kizuizini Aung San Suu Kyi aachiliwa huru, Ban akaribisha hatua hiyo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua ya kuachiliwa huru kwa kiongozi anayepigania demokrasia nchini Myanmar Aung San Suu Kyi.

Ban Ki-moon amesema utu na ujasiri wake umekuwa ni wa kutia hamasa kwa watu duniani kote.

Aung San Suu Kyi, ambaye amekuwa kuzuizini kwa miaka 15 kati ya 21 iliyopita ameachiliwa Jumamosi jioni ya leo. Su Kyi mwenye umri wa miaka 65 na mshindi ya tuzo ya amani ya Nobel amekuwa ni nembo ya kupigania demokrasia nchini Myanmar, nchi ambayo imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu mwaka 1962.

Akikaribishwa kuachiliwa kwake Katibu Mkuu amesema ni jambo la kujitia kwamba hakushirikishwa kwenye uchaguzi mkuu wa karibuni nchini humo. Ameutaka uongozi Myanmar kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa waliosalia.