Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukishirikiana bega kwa bega tutafikia malengo ya milenia Tanzania:Pinda

Tukishirikiana bega kwa bega tutafikia malengo ya milenia Tanzania:Pinda

Viongozi wa nchi 20 zilizoendelea kiuchuni duniani yaani G-20 wamehitimisha mkutano wa Ijumaa hii mjini seoul Korea.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka nchi hizo kunyoosha mkono zaidi katika kuzisaidia nchi masikini kufikia malengo ya maendeleo ya milenia. Kwa upande wake nchi hizo zimesema pamoja na kuzisaidia nchi masikini zinazoendelea zisibweteke na kutegemea msaada pekee katika kutimiza malengo hayo bali nazo zijikakamue na kuongeza juhudi.

Nyingi zinafanya hivyo ikiwemo Tanzania. Waziri mkuu wa serikali  ya nchi hiyo Mizengo Pinda amemweleza Flora Nducha mkuu wa idhaa hii kuwa wamepiga hatua na wana imani watafikia baadhi ya malengo hayo wasikilize.