Skip to main content

UM nchini Ivory Coast wahalalisha matokeo ya uchaguzi mkuu

UM nchini Ivory Coast wahalalisha matokeo ya uchaguzi mkuu

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast Young-Jin Choi amehalalisha matokeo ya uchaguzi wa hivi majuzi uliofanyika nchini Ivory Coast na kusema kuwa hakuna dosari au udanganyifu ambao ungevuruga matokeo kwa njia moja au nyingine.

Akiongea mjini Abidjan Choi amesema kuwa njia iliyotumika katika kuthibitishwa kwa matokeo ya mwisho ilifanywa kwa haki na uwazi. Awamu ya pili ya uchaguzi huo kati ya rais Laurent Gbagbo na mshindani wake Alassane Ouattara unatarajiwa kuandaliwa tarehe 28 mwezi huu.