Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahutubia viongozi wa mataifa ya G20 kwenye siku ya mwisho ya mkutano wao

Ban ahutubia viongozi wa mataifa ya G20 kwenye siku ya mwisho ya mkutano wao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa viongozi wa mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi ya G20 kulifanya suala la maendeleo kuwa muhimu.

Ametoa wito kwa viongozi wa mataifa hayo kutimiza ahadi walizotoa katika kutimiza malengo ya milnnia na kuyabadili maneno kuwa vitendo. Amesema kuwa ulimwengu uko makini huku wengi wakiwa na hasira na kuumia. Ameongeza kuwa ni jukumu vviongozi hao kuonyesha kuwa wanaelewa na wako tayari kuchukua hatua. Wakati huo huo shirika la kazi duniani ILO limetoa wito kwa mataifa ya G20 kuhakikisha kuwa kuna ajira . Mkurugenzi wa ILO Juan Somavia, amaetoa wito kwa vionngozi hao kutekeleza ahadi na kubuni nafasi bora za ajira kama moja ya njia ya kuimarika kwa ulimwengu. Mkutano huo uliondaliwa mjini Seoul nchini Korea Kusini ulikubaliana kuwa kubuni nafasi bora za ajira ndiyo nguzo ya kuimarika kwa uchumi duniani.