Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umezindua juhudi mpya za kukabiliana na kipindupindu nchini Haiti

UM umezindua juhudi mpya za kukabiliana na kipindupindu nchini Haiti

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa huenda zaidi ya watu 200,000 wakapata maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu nchini Haiti kwa muda wa miezi sita ijayo.

WHO pia linaonya kuwa huenda maambukizi ya ugonjwa huo yakashinda nguvu jitihada za kukabiliana nao . Hadi sasa vifo 724 vilivyosababishwa na ugonjwa wa kipindupindu vimeripotiwa nchini Haiti wakati watu 11,124 wakipata matibabu hospitalini. Gregory Hartl ni kutoka shirika la WHO: (SAUTI YA GREGORY HARTL):