Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki izingatiwe katika uwakilishi Baraza la usalama:Afrika

Haki izingatiwe katika uwakilishi Baraza la usalama:Afrika

Nchi hizo ambazo zinaunda jumuiya ya nchi zisizofungamana na upande wowote, iliyoundwa katika miaka ya 1960 wakati kulikozuka vita baridi, zinataka kuwepo kwa mageuzi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kukaribisha uwakilishi sawa wa kimabara.

Nchi hizo zinataka nchi za afrika kupatiwa nafasi ya kuwa mwanachama wa kudumu kwenye Baraza la Usalama.

Balozi wa Misri Maged Abdelaziz akiwasilisha hoja hiyi mbele ya Baraza la Usalama amesema kuwa ulimwengu unatambua namna afrika inavyokosa haki kutokana na mazingira ya kihistoria, lakini hata hivyo wakati umefika kwa bara hilo kupewa nafasi ya uwakilishi kwenye chombo hiko