Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Latin America yapiga hatua kubwa juu ya wakimbizi duniani

Latin America yapiga hatua kubwa juu ya wakimbizi duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limekaribisha kwa mikono miwili azimio linalotaka kulindwa na kuheshimiwa kwa wakimbizi katika eneo la nchi za Latini Amerika.

Kamishna Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres amewaambia waandishi wa habari kuwa azimio hilo linalofahamika kama azimio la Brasilia juu ya kulindwa kwa wakimbizi na wale wasiokuwa na makazi katika eneo la Amerika ni hatua ambayo inatoa matumaini makubwa.

Nchi zipatazo 18 zilizoko kwenye ukanda huo wa Amerika zimepitisha azimio hilo kwenye mkutano wao uliofanyika huko Brasilia mji mkuu wa Brazil. Zinataka kuzingatiwa kwa ustawi wakimbizi pamoja na wale wanaokosa makazi maalumu kwa sababu mbalimbali.

UNHCR imesema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwani imeonyesha utashi wa kisiasa wenye shabaya ya kutaka kukabiliana na matatizo ya wakimbizi kwa ushirikiano zaidi.

End