Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zichukuliwe kuwalinda wanawake na utoaji mimba

Hatua zichukuliwe kuwalinda wanawake na utoaji mimba

Wito umetolewa kwa hatua zaidi kuchukuliwa kuwalinda wanawake kutokana na hatari za utoaji mimba usio salama.

Akihutubia mkutano unaochunguza kiwango cha tatizo hilo barani afrika ambapo utoaji mimba milioni 5.5 usio salama unafanyika kila mwaka, mkurugenzi wa kituo cha jinsia na maendeleo ya kijamii barani Afrika Thokozile Ruzvidzo amesema kuwa hatua kadha zimepigwa kuhusu afya ya wanawake na vifo vinavyotokana na uzazi na utoaji mimba usio salama lakini akaongeza kuwa jitihada za kutimiza ahadi lazima ziwepo.

Inakadiriwa kuwa wanawake 36,000 wa umri wa kwenda shuleni wanakufa kila mwaka kutokana na utoaji mimba usio salama barani afrika. Mkutano huo wenye kauli mbiu " kutimiza ahadi yetu" unawaleta pamoja wataalamu wa afya na watunzi wa sera kutoka kote Afrika kutambua afya ya uzazi kama suala tata barani.