Baraza la usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Iraq

11 Novemba 2010

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mfululizo wa matikio ya kigaidi nchini Iraq, ambapo leo tena kumeshuhudiwa mlipuko mkubwa ukitokea kwenye mji mkuu Baghdad na kupoteza maisha ya watu kadhaa.

Mamia ya wengine wamejeruhiwa vibaya. Baraza hilo la usalama limeeleza kusikitishwa kwake kutokana na matukio hayo ambayo mengi yao yamekuwa yakilenga maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo kwenye mikusanyiko ya sehumu za ibada.

Katika taarifa yake juu ya kadhia hiyo, Balozi wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa ambaye nchi yake inashikilia kiti cha urais wa mzunguko Mark Lyall Grant amesema ameyalaani mashambulizi hayo hasa yale yanayofanywa kwa misingi ya kidini.

Hata hivyo ameelezea matumaini yake kwa wananchi wa Iraq kuwa wataendekea kushikamana na kuwa wamoja kwenye kipindi hiki.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter