Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasudan 5000 wakimbilia Kenya kuepuka machafuko

Wasudan 5000 wakimbilia Kenya kuepuka machafuko

Watu takribani 5000 kutoka Sudan Kusini wamevuka mpaka na kuingia nchini Kenya wakikimbia machafuko na ukame.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema baadhi ya watu waliokimbilia Kenya wanahofia machafuko ya kuelekea kura ya mani ambayo itaamu endapo Sudan Kusini ijitenge na kuwa taifa huru ama la hapo Januari mwakani.

Endapo hali hii itaendelea basi itageuza moja ya mipango mikubwa kabisa ya Umoja wa Mataifa iliyoshuhudia zaidi ya watu nusu milioni wa Sudan Kusini wakirejea nyumbani miaka mitano iliyopita. Yusuf Hassan ni msemaji wa UNHCR mjini Nairobi.

(SAUTI YA YUSUF HASSAN)

Yusuf anasema wengi wao wapo Kakuma kambi ambayo ni kubwa na ina wakimbizi wengi wa Sudan Kusini ambako wanapata msaada wa kutosha ikiwemo chakula, msaada wa malazi, afya na elimu.