Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya wasichana wawili Somalia

UM walaani mauaji ya wasichana wawili Somalia

Wataalamu binafsi sita wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali mauji ya kikatili ya karibuni yaliyofanywa hadharani dhidi ya wasichana wawili wa katikati mwa Somalia.

Wataalamu hao wanasema mauaji hayo ni ushahidi wa kusikitisha wa matatizo ya haki za binadamu yanayoikabili nchi hiyo. Wataalamu hao wamesema tulipatwa na butwaa baada ya kufahamu mauaji hayo yanayodaiwa kufwaywa hadharani na wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab. Wasichana wawili waliuawa kikatili mbele ya mamia ya wakazi wa Beledweyne Oktoba 27.

Kundi hilo limeongeza kuwa linaungana na watu wa Somalia kulaani muaji hayo na limezitaka pande zote husika katika vita vya Somalia kusita kutekeleza vitendo vya mauaji, utesaji, kuwaponda watu mawe, kuwakata viungo na kuwazika wakiwa hai, ikiwa ni pamoja na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu unaojumuisha uhuru wa dini.

Wataalamu hao walioteuliwa na baraza la haki za binadamu wamesema wanahofia makundi kama Al-Shabaab wanairudisha Somalia katika zama za kale.