Polio yakatili maisha ya watu 100 nchini Congo
Shirika la afya duniani WHO linasema mlipuko wa ugonjwa wa polio umeuwa watu takribani 100 nchini Congo Brazzaville.
Mlipuko huo umejikita zaidi katika mji wa bandari wa Pointe Noire ambako visa 226 vya polio vimeripotiwa. WHO inasema ugonjwa huo unasambaa haraka na unawaathiri zaidi vijana.
Olivier Rosenbauer kutoka WHO kitengo cha mradi wa kutokomeza polio anasema kampeni kubwa ya chanjo inayowalenga watu milioni 3 itafanyika Congo na kwenye mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Angola.
(SAUTI YA OLIVIER ROSENBAUER)
Polio ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambavyo hushambulia mfumo wa neva na kusababisha kupooza katika muda wa masaaa tuu.Hakuna tiba ya ugonjwa huo lakini unaweza kukingwa kwa njia ya chanjo.