Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malengo ya maendeleo ya milenia yanaweza kufikiwa kukiwa na msaada na ari ya kisiasa:Ban

Malengo ya maendeleo ya milenia yanaweza kufikiwa kukiwa na msaada na ari ya kisiasa:Ban

Msaada mkubwa wa kisiasa unahitajika ili kufikia malengo ya maendeleo ya milenia yaliyowekwa na viongozi wa dunia mwaka 2000 ya kutokomeza umasikini, elimu ya msingi kwa wote na kupambana na maradhi ifikapo 2015.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon mjini Seoul Korea ambako anahudhuria mkutano wa mataifa 20 yaani G-20 yanayoongoza kiuchumi duniani. Ban amesema licha ya mashaka yaliyopo bado malengo hayo yanaweza kufikiwa kabla ya muda wa mwisho wa mwaka 2015.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban pia amejadili na Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma masuala mamblimbali ikiwemo mkutano huo wa G-20, maendeleo, malengo ya milenia, mabadiliko ya hali ya hewa, matatizo yanayoikabilia Afrika na jopo la kimataifa lililoundwa na la Katibu Mkuu kushughulikia maendeleo endelevu.

Pia ameipongeza afrika ya Kusini kwa kuchaguliwa kuwa kama mjumbe asiye wa kudumu kwenye baraza la usalama hasa wakati huu ambao ni nyeti kwa Afrika na dunia kwa ujumla.