Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rwanda yachangia dola milioni 1 kwa Global Fund

Rwanda yachangia dola milioni 1 kwa Global Fund

Rwanda imetoa msaada wa dola milioni moja kwa mfuko wa kimataifa yaani Global Fund kwa ajili ya kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria.

Rais Paul Kagame wa taifa hilo la afrika ya Kati amesema hata kama ni uwekezaji mdogo unaweza kuokoa maisha na kuinua uchumi kwa uzalishaji kupitia ongezeko la nguvu kazi. Mfuko huo ambo ulianzishwa mwaka 2002 , umeshapokea msaada wa ahadi ya dola bilioni 11.7 kwa ajili ya mwaka 2011 hadi 2013.

Mipango na miradi mbalimbali  inayofadhiliwa na mfuko huo imekuwa ikitoa matibabu ya ukimwi kwa watu milioni 7 na kutoa vyandarua milioni 122 venye dawa ili kuzuia malaria.