Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zaidi zipige vita mabomu ya vishada:Migiro

Nchi zaidi zipige vita mabomu ya vishada:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amezipongeza nchi ambazo tayari zimeanza kutekeleza mkataba wa upigaji marafuku matumizi ya mabomu ya vishanda, lakini ametaka nchi nyingine ambazo hazijafanya hivyo kuunga mkono juhudi hizo.

Akizungumza kwenye kongamano la kwanza linalofanyika huko Laos, Vientiane kuhusiana na matumizi ya mabomu hayo ya vishada, Migiro amesema kuwa, kuasisiwa kwa mkataba huo ni hatua muhimu ambayo inatoa uhai kwa sheria za kimataifa zinazohusika na usalama wa binadamu. George Njogopa na taarifa zaidi(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Naibu Katibu hiyo ameseama hatua ya kupiga marafuku hali yoyoye ya utumiaji, utengenezaji pamoja na usafirishaji wa mabomu hayo, ni jambo lisolohitaji mjadala tena. Pamoja na mambo mengine, sheria hiyo ya uzuiaji wa matumizi mabomu hayo, inataka kuwepo kwa fidia kwa waathirika wa mabomu hayo bila kusahau nchi zao. 

Mkataba huo umeanza kufanya kazi tangu August mosi mwaka huu na tayari nchi 108 zimesaini kuutambua. Lakini nchi 46 ndizo zilizoidhinisha sheria hiyo ianze kufanya kazi.