Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa DRC waliofukuzwa Angola walibakwa:OCHA

Wakimbizi wa DRC waliofukuzwa Angola walibakwa:OCHA

Wakimbizi wanaokadiriwa kufikia elfu saba wamewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipindi cha miezi miwili baada ya kutimuliwa nchini Angola.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA wengi wamebakwa wakati wa mchakato wa kufukuzwa, Umoja wa Mataifa ulifahamu kuhusu ukatili huo Oktoba 23 kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali baada ya kushuhudia watu zaidi ya elfu sita waliowasili kati ya Septemba na Oktoba kwenye jimbo la Kasai Magharibi na wengine 322 mjini Tembo jimbo la Bandundu.

Wakimbizi hao wengi ni raia wa Congo na baadhi kutoka mataifa mengine ya Afrika. Kati yao wanawake 99 na wanaume 15 wamearifu kubwakwa, haki zao za binadamu kukiukwa na kunyanyaswa. Maurizio Giuliano ni msemaji wa OCHA nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

(SAUTI YA MAURIZIO GIULIANO)

Kutimuliwa kwa wakimbizi kutoka katika nchi zote mbili sio jambo jipya na linatokana na umasikini na ukosefu wa ajira, 2009 maelfu ya wakimbizi walitimuliwa katika nchi zote mbili.