UNAMID inafanya kazi nzuri kuwalinda raia Darfur :Uingereza

UNAMID inafanya kazi nzuri kuwalinda raia Darfur :Uingereza

Kazi ya vikosi vya muungano vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika Darfur UNAMID imepongezwa na waziri wa maendeleo ya kiamatifa wa Uingereza Andrew Mitchell.

Ameelezea matumaini yake kwamba majadiliano yanayoendelea ya Doha kuhusu makubaliano mapya ya amani ya Darfur yatazaa matunda ili kuimarisha zaidi hali ya jimbo hilo na kuleta amani ya kudumu.

Akizungumza mjini El Fasher makao makuu ya Darfur Kaskazini katika mwisho wa ziara yake ya siku moja Darfur bwana Mitchell amesema doria inayofanywa na UNAMID katika makambi na kuwasinzikiza kina mama kwenda kuokota kuni ni hatua zinazohakikisha kuna usalama na kuwalinda raia katika makambi.

Ameongeza kuwa kuzunguka katika makambi kunaonyesha umuhimu wa kazi inayofanywa na Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika katika kuwalinda watu walio katika hatari , wanawake , watoto na wakimbizi wote kwa ujumla.