Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migiro ahudhuria mkutano wa mabomu mtawanyiko Laos

Migiro ahudhuria mkutano wa mabomu mtawanyiko Laos

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amewasili mjini Vientiane Laos kabla ya mkutano wa kupiga marufuku mabomu yanayotawanyika ikiwa ndiyo nchi ya kwanza anayozuru kati ya nchi tatu zilizo kwenye mpango wa ziara yake zikiwemo Lebanon na Ethiopia.

Bi Migiro anamwakilisha katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye mkutano wa kwanza wa mataifa yaliyo kwenye makubalino ya kupiga marufuku mabomu yanayotawanyika unaong'oa nanga hii leo na kujadili kutekelewzwa kwa makubalino hayo yanayopiga marufu matumizi , utengezaji na bishara ya mabomu yatawanyikayo.

Mkataba huo ulianza kutumika tarehe mosi mwezi Agosti mwaka 2010 na hadi sasa umepata sahihi kutoka nchi 108 . Hadi mwishoni mwaka 2009 visa 16,816 vya mabomu yanayotawanyika viliripotiwa lakiji hata hivyo huenda visa hivyo vikawa hata zaidi ya 85,000 kote duniani.