Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yazuka Sahara Magharibi wakati mazungumzo yakianza New York

Mapigano yazuka Sahara Magharibi wakati mazungumzo yakianza New York

Wakati mapigano makali yakizuka kwenye kambi ya Sahara Magharibi nchini Morocco na kusababisha watu wasiopungua watano kufariki dunia pande hizo zinazohasimiana zinaanza kukutana leo New York Marekani kwa mazungumzo ya kujadili mustakbali wa eneo hilo.

Mazungumzo hayo yasiyo rasmi, yanafanyika chini ya ushawishi wa Umoja wa Mataifa ambayo pia yanawahusisha wawakilishi toka nchi jirani za Algeria na Mauritania. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo Christopher Ross.ametaka pande hizo zinazohasimiana kujiepusha na vitendo vya ghasia.

Makumi ya watu wameripotiwa kujeruhiwa katika machafuko hayo ambayo baadaye yalitoka kwenye kambi moja na kuenea kwenye mitaa ya mji wa La'ayun. Mgogoro wa kupinga utawala wa Morocco huko Sahara Magharibi umedumu kwa miaka 35 sasa. Chama cha Polisario kinachopigania kujitenga Sahara Magharibi, kimelalamikia vikali hatua ya wanajeshi wa serikali ya kuvamia kambi hiyo.