Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kujadili sheria kwa makampuni binafsi ya ulinzi

UM kujadili sheria kwa makampuni binafsi ya ulinzi

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya matumizi ya askari mamluki litafanya ziara nchini Afrika ya Kusini kuanzia kesho Novemba 10 hadi 19 ili kuangalia sheria na mfumo uliopo wa kusimamia shughuli za jeshi na makampuni binafsi ya ulinzi.

Kwa miaka mingi Afrika ya Kusini imekuwa kituo cha mafunzo kwa ajili ya jeshi na makampuni binafsi ya ulinzi, na matokeo yake imekuwa moja ya nchi chache kuchukua hatua muafaka, zikiwemo sheria za kushughulikia shughuli za makampuni hayo.

Mwenyekiti wa kundi hilo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa Alexander Nikitin ambaye atakwenda pia mjini Cape Town na Pretoria amesema nia yao ni kutanabahi athari za shughuli hizo katika masuala ya haki za binadamu na juhudi za kuhakikisha uwajibikaji kwa wavunja sheria. Jayson Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)