Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindupindi na kimbunga vimeathiri Haiti:OCHA

Kipindupindi na kimbunga vimeathiri Haiti:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema majanga mawili makubwa yaliyoikumba Haiti hivi karibuni yamesababisha athari kubwa.

Kipindupindu na kimbunga Tomas kwa pamoja vimesababisha vifo zaidi ya 550. Takwimu rasmi zinasema watu 21 wamekufa na kimbunga Tomas, 6610 wameachwa bila makazi na wengine 48,000 imebidi wahamishwe huku 24,200 kati yao wakipata hifadhi katika makambi 75 ya muda. Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

Kwa upande wa kipindupindu wizara ya afya ya Haiti inasema watu 54 wameshafariki dunia hadi sasana wengine 8138 wamelazwa hospitali kutokana na ugonjwa huo. Vituo 14 vya tiba vimewekwa ili kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu na mipango maalumu ya kuarifu visa vipya na kuzuia kuzuka tena kwa ugonjwa huo imetayarishwa katika juhudi za kuisaidia wizara ya afya ya nchi hiyo.