Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Meli za kivita pekee haziwezi kumaliza tatizo la uharamia pwani ya Somalia laambiwa baraza la usalama

Meli za kivita pekee haziwezi kumaliza tatizo la uharamia pwani ya Somalia laambiwa baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili tatizo la uharamia katika pwani ya Somalia na bahari ya Hindi.

Akizungumza kwenye kikao hicho mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu katika masuala ya kisiasa Lynn Pascoe amesema hali inatisha kwani kwa mujibu wa shirika la kimataifa la masuala ya ubaharia IMO meli 20 na mabaharia na abiria 438 wanashikiliwa na maharamia tangu tarehe 4 Novemba mwaka huu.

Amesema hili ni ongezelo la takribani utekaji wa watu 100 katika chini ya mwezi mmoja, na ametoa witi wa kuachiliwa mara moja watu wote waliotekwa na maharamia hao. Amesema uharamia huo uanathari kubwa sio kwa Afrika ya mashariki tuu bali dunia nzima

(SAUTI YA LYNNY PASCOE)

Ameongeza kuwa mbali ya kuweka maisha ya wanaowateka hatarini maharamia hao wanakuchukua hatari kubwa kufanya hivyo lakini pia wamegeuza utekaji wa meli na watu biashara kwa kudai kikombozi. Pascoe amesema nchi wanachama wameweka mikakati ya kukabiliana na uharamia huo ikiwemo kuweka meli za doria.