Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yakagua mahitaji baada ya kimbunga kuikumba Haiti

UNICEF yakagua mahitaji baada ya kimbunga kuikumba Haiti

Makundi kutoka shirika la kuwadumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF yanaendelea kukagua mahitaji kwenye mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince na sehemu zingine zilizokumbwa na kimbunga Tomas yanapojiandaa kupeleka misaada kwenye maeneo yaliyoathirika.

Mvua kubwa kutoka kwa kimbunga hicho zilisababisha mafuriko katika sehemu nyingi za Haiti huku mafuriko makubwa yakiripotiwa katika eneo la Gonaives kaskazini mwa mto Artibonite.

George Njogopa na taarifa zaidi. (SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)