Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito wa kutaka kuachiliwa kwa mfanyikazi wa UNAMID watolewa

Wito wa kutaka kuachiliwa kwa mfanyikazi wa UNAMID watolewa

Katibu wa idara inayohusika na masula ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na mratibu wa huduma za dharura Valery Amos ametoa wito wa kutaka kuachiliwa mara moja kwa mfanyikazi wa kwa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na cha Muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur UNAMID aliyetekwa nyara siku 30 zilizopita.

Akiongea na waaandishi wa habari baada ya kufanya mkutano na mmoja wa viongozi wa jimbo la Darfur Amos amesema kuwa mkutano wao ulizungumzia masuala yakiwemo ya usalama ya wafanyikazi wa mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu na ushirikino kati yao na utawala kushughulikia changamoto zinazowakumba wenyeji wa jimbo hilo.