Skip to main content

Kituo kinachohusika na masuala ya uchumi wa fedha katika mashariki ya kati chaanzishwa

Kituo kinachohusika na masuala ya uchumi wa fedha katika mashariki ya kati chaanzishwa

Kituo maalumu kitakachoshughulikia masuala ya uchumi na fedha katika eneo la mashariki ya kati, kipo mbioni kuanzishwa kufuatia makubaliano yaliyofikiwa baina ya fuko la fedha duniani IMF na Serikali ya Kuwait.

Kituo hicho ambacho makao yake makuu yanatazamiwa kuwa Kuwait, kitakuwa na kazi ya kutoa mafunzo kwa maafisa wa serikali kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya nchi za kiarabu.

Masuala ya upangaji wa sera za kiuchumi na utekelezaji wake ni baadhi ya maeneo ambayo kituo hiki kitazingatia.

Kinatazamiwa kuzinduliwa rasmi May 2011