Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga Tomas chakaribia fukwe ya Haiti tahadhari zachukuliwa

Kimbunga Tomas chakaribia fukwe ya Haiti tahadhari zachukuliwa

Wakati kimbunga aina ya Tomas kikikaribia kuipiga fukwe wa Haiti, Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanaza opereshini maalumu kuhakikisha kwamba magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu hakienei kwenye eneo hilo.

Kimbunga hicho kinatazamia kupiga mji wa Jérémie uliopo upande wa magharibi wan nchi hiyo na kunauwezekano mkubwa mji mkuu wa Port-au-Prince ukasalimika na dhoruba hiyo. Hata hali ya mvua kali iliyoambatana na upepo mkali ulizua hali ya usalama kwa watu zaidi ya milioni 1.3 walioko kwenye mji mkuu ambao hawana makazi maalumu.

Maafisa kadhaa wameelezea wasiwasi wao wa watu hao kuwa hatarini kukubwa na magonjwa hayo ya mlipuko. Hapo alhamisi IOM ilifanikiwa kuhamisha zaidi ya watu 2,000 kutoka katika makambi kadhaa na kuwapeleka kwenye hospitali moja, wengi wao wakiwa watoto na kina mama.