Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuandaa kongamano la ujenzi mpya wa Pakistan baada ya mafuriko

UM kuandaa kongamano la ujenzi mpya wa Pakistan baada ya mafuriko

Shirika la umoja wa mataifa linaloratibu misaada ya usamaria mwema UNOCHA likishirikiana na benki ijulikanayo Pakistan JS Bank Limited linaandaa kongamano maalumu kwa ajili ya kuijenga upya Pakistan

Kongamano hilo ambalo linafanyika jumatatu ijayo Novemba 8, linatazamiwa kuwaleta pamoja jumla ya wajumbe 500 kwa ajili ya kufanikisha wa ujenzi mpya wa eneo la Sindh huko Karachi eneo ambalo liliathiriwa vibaya na mafuriko ya hivi karibuni.

Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yametia nguvu kwenye ufanikishaji wa kongamano hilo. Baadhi ya mashirika hayo ni pamoja na WFP, WHO, UNICEF, UNHABITAT na IOM. Watu zaidi ya milioni 18 wameathiriwa na mafuriko hayo na kati yao milioni 14 wapo kwenye hitajio la haraka zaidi la kupatiwa huduma za usamaria wema.