Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yaliambia baraza la haki za binadamu haitesi watu

Marekani yaliambia baraza la haki za binadamu haitesi watu

Naibu waziri katika wizara ya demokrasia , haki za binadamu na leba nchini Marekani Michael Posner amesema kuwa nchi yake inatekeleza haki kulingana na sheria zinazolinda haki za binadamu.

Akiwasilisha ripoti kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Posner hata hivyo aliliambia baraza hilo kuwa Marekani kwa sasa inashughulikia mizozo nchini Afghanistan, Iraq pamoja na kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Amesema kuwa Marekani inaheshimu katiba na sheria zote za nchi akiongeza kuwa hakuna maeneo yasiyokuwa na sheria.