Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedha bado ni tatizo siku 100 baaya ya mafuriko Pakistan

Fedha bado ni tatizo siku 100 baaya ya mafuriko Pakistan

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa siku 100 baada ya mafuriko kuikumba Pakistan kwa sasa mamilioni ya watu wanahitaji usaidizi wa dharura.

Linasema kuwa karibu watu milioni 14 wanahitaji misada ya kibinadamu. UNICEF linasema ukosefu mkubwa wa fedha za kufadhili huduma zake za dharura kumeathiri mipango yake ya kuokoa maisha kwa watoto na familia.

Linasema kuwa limepokea dola milioni 133 katika ya dola milioni 252 lilizo omba likisema huduma kama vile kuwajiri wahudumu wa afya , elimu, usalama , maji na lishe huenda vikakosa. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)