Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa dharura wahitajika kukabili kimbunga Tomas:OCHA

Msaada wa dharura wahitajika kukabili kimbunga Tomas:OCHA

Umoja wa Mataifa unatoa wito wa misaada zaidi ya dharura pamoja na vifaa kwa taifa la Haiti wakati kimbunga Tomas kinapokaribia kuweasili nchini humo.

Inakadiriwa watu 500,000 huenda wakaathiriwa na kimbunga hicho. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa huenda hali mbaya ya kimazingira iliyo kwenye sehemu nyingi za nchi na mvua pamoja na mafuriko vitakayosababishwa na kimbunga hicho vikachochea kusambaa zaidi kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Vikosi vya wjeshi wa Marekani vilivyo nchini Haiti vinajiandaa kutoa usaidizi katika maeneo yatakayoathirika. Elizabeth Byres ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa limeweka tayari misaada ya dharura ya vyakula kwenye vituo 32 kote nchini likiwa na chakula kinachoweza kulisha watu milioni moja kwa majuma sita. Pia mashua kubwa zimewekwa tayari kuweza kusafirisha chakula ikiwa barabara hazitapitika.