Skip to main content

Polio yaripotiwa kuzuka DR Congo:WHO

Polio yaripotiwa kuzuka DR Congo:WHO

Mkurupuko wa ugonjwa wa Polio umeripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku visa ya maambukizi 120 na vifo 58 vikiripotiwa.

Nusu ya visa vya ugonjwa huo vimeripotiwa kwa muda wa siku kumi zilizopita. Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa serikali ya DRC imeuatadharisha umma kuhusu ugonjwa huo na kuazisha shughuli za dharura kwa usaidizi wa mashirika ya WHO , UNICEF na US CDC huku kukitarajiwa kampeni tatu za kutoa chanjo kote nchini. Oliver Rosenbauer ni afisa wa WHO

(SAUTI YA OLIVER ROSENBAUER)

WHO linasema kuwa ni muhimu kwa nchi zilizo kwenye kanda ya Afrika ya kati na pembe ya Afrika kuwa macho ili kuweza kutambua dalili zozote za ugonjwa huo . Limeongeza kuwa wasafiri kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watahitaji kuchanjwa dhidi ya ugonjwa huo.