Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watangaza duru nyingine ya mazungumzo Sahara Magharibi

UM watangaza duru nyingine ya mazungumzo Sahara Magharibi

Awamu nyingine ya mazungumzo kati ya pande zinazo zozana Sahara Magharibi itafanyika mjini New York juma lijalo kwa mwaliko wa Umoja awa Mataifa.

Msemaji wa Umoja wa mataifa Martin Nesirky anasema kuwa wajumbe wanaowakilisha pande mbili husika zikiwemo Morocco na Frente Polisario yakiwemo mataifa jirani ya Algeria na Mauritania watakusanyika katika kisiwa cha Long kwa mkutano wa siku mbili kati ya tarehe nane na tisa mwezi huu.

Umoja wa Mataifa umekuwa kwenye mstari wa mbele katika juhudi za utatuzi wa mzozo wa Sahara magharibi tangu mwaka 1976 wakati kulipozuka mapigano kati ya Morocco na eneo la Frente Polisario kufuatia kukamilika kwa utawala wa kikoloni wa Hispania katika ene la Frente Polisario.

Morocco ilikuwa imewasilisha mpango wa kulitawala eneo la Frente Polisario wakati msimamo wa eneo hilo ukiwa kwamba hali yake iamuliwe na kura ya maoni itakayoamua uhuru wake.