UM waeleza matatizo yanayokumba miji duniani
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililo na jukumu la kuboresha miji ameelezea changamoto zinazokumba miji sehemu mbali mbali duniani akisema kuwa miji mingi ina idadi kubwa ya wakaazi ambao haina uwezo wa kuwahudumia.
Akigusia baadhi ya masuala atakayoshughulikia kama katibu wa shirika la makaazi la Umoja wa Mataifa UN HABITAT, Joan Clos amewaammbia waandishi wa habari mjini New York kuwa hata kama miji ina viwanda na biashara vilivyo asilimia kubwa ya utajiri wa dunia bado haina uwezo wa kuhudumia idadi ya watu inayoendelea kuongezeka .
Clos amesema kuwa huku miji kwenye nchi zinazoendelea ikiendelea kukumbwa na shida zikiwemo za umaskini, ukosefu wa maendeleo, huduma duni za afya, za elimu na za kiusalama pia changamoto mpya mijini kwenye nchi maskini na tajiri zinazidi kuongezeka.
Clos ameongeza kuwa shirika la UN-HABITAT litakuwa likitafuta suluhisho kwa changamoto zinazokabili serikali za mijini kwenye juhudi zao za kutafuta suluhisho kwa changamoto hizo.