Skip to main content

Muasi wa Rwanda apelekwa The Hague kujibu mashitaka

Muasi wa Rwanda apelekwa The Hague kujibu mashitaka

Kiongozi wa uasi nchini Rwanda amekamatwa na kupelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu.

Kiongozi huyo muasi wa Rwanda anatazamiwa kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa ICC kuyakabili mashtaka dhidi yake, kufuatia uamuzi wa mahakama moja ya ufaransa kukubali kumkabidhi the Hague.

Callixte Mbarushimana anatuhumiwa kuhusika kwa makosa 11 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikiwa pamoja na uhalifu wa kivita, na ukatili dhidi ya binadamu. Alikamatwa na mamlaka za dola nchini Ufaransa mwezi uliopita. Hata hivyo ameyakana mashtaka hayo.