Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awataka viongozi wa Guinea kujiepusha na ghasia

Ban awataka viongozi wa Guinea kujiepusha na ghasia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa Guiene kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa wiki.

Bwana Ban hata hivyo amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa na pande zote nchini humo kuruhusu duru ya pili ya uchaguzi ifanyike November 7. Ametaka pande zote kuheshimu tarehe hiyo iliyowekwa ya upigaji kura

Ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuzuka kwa matukio ya ghasia ambayo yamewalazimu baadhi ya watu kuanza kuhama makazi yao na kwenda sehemu nyingine ya maeneo ya mbali.