Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la UM limetakiwa kuliunga mkono baraza la haki za binadamu

Baraza la UM limetakiwa kuliunga mkono baraza la haki za binadamu

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limetakiwa kutoa msaada zaidi ili kulisaidia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Baraza la haki za binadamu liliundwa mwaka 2006 kwa jukumu la kuimarisha na kuendeleza uchagizaji na kulinda haki za binadamu duniani kote. Baraza kuu limeelezwa bila msaada na fedha za kutosha itakuwa vigumu kwa baraza la haki za binadamu kutekeleza wajibu wake ipasavyo. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limetakiwa kutoa msaada wa kifedha na vitendea kazi kwa Baraza la Umoja huo linalohusika na masuala ya haki za binadamu. Akiwasilisha ripoti ya kwenye makao makuu ya baraza hilo huko Geneva, Balozi Sihasak Phuangketkeow ameliambia Baraza hilo kuwa kunahitajika msaada zaidi wa vitendea kazi pamoja na fedha ili kuzikabili changamoto zinazohusiana na masuala ya haki za binadamu.

Balozi huyo amesema kuwa hali ilivyo kwa sasa, haitoa fursa kwa Baraza kuu kufanya maamuzi yoyote mpaka inapofika mwishoni mwa mwaka jambo ambalo amesema kuwa linaathiri kwa kiwango kikubwa utendaji kazi wa baraza hilo la haki za binadamu.