Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asia na Pacific wakutana kujadili haki za watoto

Asia na Pacific wakutana kujadili haki za watoto

Mawaziri na maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi 28 za Asia na Pacific wanakutana Beijing China leo kwa ajili ya mkutano wa kuboresha ushirikiano kwa ajili ya haki za watoto.

Mkutano huo utakaokamilika Novemba sita umeandaliwa na shirikisho la wanawake wa Uchina, kamati ya taifa ya wanawake na watoto, wizara ya biashara ya watu wa Uchina kwa msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Maafisa wa serikali ya Uchina na UNICEF pia wanahudhuria mkutano huo. Kwa pamoja nchi zinazoshiriki mkutano huo zinawakilisha watoto bilioni moja sawa na asilimia 53 ya watoto wote duniani.

Maafisa hao wa serikali watajikita katika masuala matatu muhimu , kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, kuboresha maisha ya watoto kwa kupunguza athari za majanga, na kulinda na kuheshimu haki na maisha ya watoto. Mada hizo zimechanguliwa kutokana na kwamba ni jambo la kawaida katika nchi hizo na wana hofu kwamba zisiposhughulikiwa athari zake zitakuwa kubwa.