Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maharamia wa Kisomali bado ni tatizo kubwa:Ban

Maharamia wa Kisomali bado ni tatizo kubwa:Ban

Shughuli za utekaji meli zinazofanywa na mahramia wa Kisomali kwenye pwani ya Somalia zimeongezeka licha ya juhudi zinazofanyika kuwazuia.

Meli za kiamataifa za doria kwenye pwani ya Somalia zimekuwa zikiingilia mra kwa mara na harakati za maharamia hao lakini tathimini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye ripoti mpya kuhusu uharamia kwenye mwabao wa bahari ya hindi inasema maharamia hao bado wanaendelea kuteka meli kwa nguvu katika pwani hiyo.

Maharamia wa Kisomali wamefanya utekaji wa meli kuwa biashara kubwa kwani hujipatia mamilioni ya dola kama kikombozi. Jayson Nyakundi na taarifa zaidi

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza hatua zilizochukuliwa za kuwafikisha mahakamani washukiwa wa uharamia na kuwafunga wanaopatikana na hatia. Ban amesema kuwa mataifa ya Kenya na Ushelisheli yametoa mchango mkubwa katika kukabiliana na uharamia.

Hata hivyo kupitia ripoti kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Ban amesema kuwa maharamia katika pwani ya Somalia wamekuwa wakali zaidi na wanaendesha shughuli zao kwenye eneo kubwa. Ni muhimu kuongeza doria baharini ili kuwazuia maharamia hao kuendesha shughuli zao sawia na kuwafikisha wanaokamatwa mahakamani.

Ameongeza kuwa hata hivyo suluhu lazima ipatikane kwa Somali yote nchi ambayo haijakuwa na serikali kwa zaidi ya miongo miwili.