Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Manusura wa utesaji kuwa mwakilishi mpya wa UM

Manusura wa utesaji kuwa mwakilishi mpya wa UM

Mtetezi wa haki za binadamu Juan E.Mendez kutoka Argentina ameteuliwa na baraza la haki za binadamu kuwa mwakilishi mpya wa masuala ya utesaji.

Mendez atakuwa na jukumu la kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu matumizi ya utesaji na ukatili mwingine, vitendo vya udhalilishaji na adhabu duniani. Akielezea matarajio katika jukumu hilo jipya Mendez amesema mimi mwenyewe ni manusura wa utesaji hivyo mtazamo wangu katika kazi hii utakuwa wa mtu ambaye ni muathirika wa suala hili.

Amesema kwa kupinga utesaji na ukatili, udhalilishaji na adhabu zinazokiuka sheria za kimataifa nita tumai kutoa mchango mkubwa katika kutekeleza haya na mika na desturi za kimataifa za kupinga masuala hayo.

Amesema vita vikubwa vinahitajika, mawazo na ari ya kisiasa pia ili kutokomeza utesaji hasa kwa watu ambao mara nyingi hatuyajuia majina wala sura zao.

Bwana Mendez katika maisha yake yote kama mwanasheria amekuwa akitetea haki za binadamu na kuelimisha, na alipokuwa akiwawakilisha wafungwa wa kisiasa aliwekwa kizuizini kwa miezi 18 nchini Argentina na mwaka 1977 alitumuliwa nchi humo na kuhamia Marekani ambako amekuwa akifanya kazi katika masuala ya sheria ikiwa ni pamoja na katika baraza la kisheria la human rights pia alikuwa kama mshauri maalumu wa UM kuhusu mauaji ya kimbari tangu mwaka 2004 hadi 2007.