Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi masikini zinapiga hatua katika maendeleo ya binadamu yasema ripoti ya UM

Nchi masikini zinapiga hatua katika maendeleo ya binadamu yasema ripoti ya UM

Ripoti ya 20 ya maendeleo ya binadamu HDR imezinduliwa leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New york.

Ripoti hiyo ilinaitwa utajiri halisi wa mataifa na njia za maendeleo ya binadamu inatathimini miaka 40 ya takwimu za maendeleo na kutanabaisha nchi ambazo zimepiga hatua katika maendeleo ya binadamu.

Maendeleo yanayoangaliwa ni yale yaliyoorodheshwa ambayo yametokana na njia isiyo ya kipato na pia inataja mikakati mitatu ambayo itakwenda sambamba na utaratibu wa jadi wa kutathimini maendeleo ya binadamu.

Bi Jeni Klugman ni mkurugenzi wa ofisi ya ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP na ni mmoja wa waandishi wakuu wa ripoti hiyo.

(SAUTI YA JENI KLUGMAN)

Naye katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo amesema maendeleo ya mwanadamu ni muhimu sana katika dunia hii.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa bado watu wa kawaida hawawezi kuwapeleka watoto wao shuleni, wanawake wajawazito hawapati huduma za afya na familia nyingi bado zinaishi kwa mashaka ya kutojua kesho watakula nini.