Uchaguzi wa Ivory Coast wapongezwa na baraza la usalama

Uchaguzi wa Ivory Coast wapongezwa na baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limewataka watu wa Ivory Coast kuendelea kuwa watulivu wakati wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika Jumapili iliyopita.

Wajumbe wa baraza la usalama wamekaribisha hatua ya kufanyika kwa uchaguzi huo na kuwapongeza watu wa Ivory Coast kwa ushiriki wao wa amani na utulivu. Wamewataka wadau wote katika uchaguzi huo kuendelea kuwa kutekeleza demokrasia, amani na uwazi katika kukamilisha mchankato mzima wa uchaguzi huo.Balozi Mark Grant wa Uingereza ndiye Rais wa baraza la usalama mwezi Novemba. Amesema

(SAUTI YA MARK GRANT)

"Wajumbe wa baraza la usalama wanatoa wito kwa wagombea wote kuendeleza mazingira ya amani na utulivu na kukubali matokeo ambayo yatatangazwa kwa mfumo maalumu iliyowekwa. Pia wamewataka wafuasi wa wagombea hao kujizuia na vitendo vyovyote vya ghasia wakati wa mchakati huu wa uchaguzi.