UNESCO kutumia michezo kuchagiza amani duniani

3 Novemba 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO limeanzisha habari mtandao kwa ajili ya kutoa msukumo kwenye masuala ya uzuiaji wa vitendo vya kikatili, kukabili ubaguzi wa rangi na hata kuwawezesha vijana.

Shirika hilo limesema kuwa linatambua ushawishi uliopo kwenye michezo hivyo kwa kutumia uga huo litaanza kutoa taarifa mtandao ambazo zitawachagisha watumiaji kwenye masuala mbalimbali. Shabaha kubwa ya mradi huo ambao unafanywa kwa ushirikiano baina ya UNESCO na chama cha kimataifa cha waandishi wa habari za michezo ni kuleta amani kupitia nguvu ya michezo.

Chapisho la kwanza linatazamia kutoka February mwakani ambalo litawekwa kwenye tovuti na kisha kusambazwa sehemu mbalimbali. Ndani ya machapisho hayo kunatazamiwa kupambwa na taarifa za hapa na pale, makala na wasifu wa wanamichezo mbalimbali.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter