Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua mpango kulinda bayo-anuai isitoweke

UM wazindua mpango kulinda bayo-anuai isitoweke

Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu makubaliano ya bayo anuai wameenzisha mkakati wa miaka kumi wenye lengo la kuzuia kupotea kwa bayo anuai duniani wakati nchi zikikubalina kuwa na mipango ya kitaifa ya kulinda mali asili itokanayo na jenetiki kati ya miaka miwili iyayo.

Mawaziri wa mazingira kutoka nchi 193 waliohudhuria mkutano wa majuma mawili wa mataifa walio wanachama wa makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu bayo anuai kwenye mji wa Nagoya nchini Japan pia waliafikia makubaliano mapya ya kugawana manufaa ya mali asili ya kijenetiki.

Kwa kutia sahihi makubaliono hayo nchi wana chama zilikubaliana kupunguza kwa nusu kutoweka kwa maeneo asili na kuongeza kwa asilimia 17 ardhi ya maeneo asili kote duniani na kwa asilimia 10 maeneo ya baharini na pwani ifikapo mwaka 2020