Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito umetolewa kupeleka utaalamu sehemu zingine duniani:UM

Wito umetolewa kupeleka utaalamu sehemu zingine duniani:UM

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa wasomi kuhakikisha kuwa kila moja amepata fursa ya kupata elimu.

Akiongea kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa wasomi mjini Shanghai Ban anasema kuwa mkutano kama huo una nia ya kuleta kuwepo kwa utaalamu kote duniani na pia kuleta tamaduni mpya.

Amesema kuwa suala kama hili linatoa mwelekeo wa kutumika kwa uvumbuzi wa wasomi hasusan sehemu ambazo UM unaendesha shughuli zake na maoni yatayosaidia kutimizwa kwa maelengo ya maendeleo ya milenia itimiapo mwaka 2015.

Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa utaandaliwa kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kati ya tarehe 18 na 19 mwezi huu.