Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya isiwatimue wakimbizi wa Kisomali:UNHCR

Kenya isiwatimue wakimbizi wa Kisomali:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema serikali ya Kenya imewataka wakimbizi 8000 wa Kisomali kwenye mji wa Mandera Kaskanizi Mashariki mwa nchi kurejea nyumbani.

Wakimbizi hao ambao wengi ni wanawake, watoto na wazee walikuwa wakiishi kwenye kambi ya muda kwenye upande wa Kenya wa mpaka baada ya kukimbia mapigano yanayoendelea mjini Bulla Hawa Somalia. UNHCR inasema kwa kuwarejesha nyumbani kwenye vita wakimbizi hao Kenya itakuwa inakiuka sheria za kimataifa za wakimbizi ambazo zinakataza kuwarejesha wakimbizi kwa nguvu.Fatoumata Lejeune Kaba ni afisa wa UNHCR Geneva.

(SAUTI YA FATOUMATA KABA)

UNHCR inasema watu wanaokimbi kutoka maeneo ya katikati na kusini mwa Somalia wako katika hatari kubwa na mahitaji yao ya ulinzi wa kimataifa ni lazima yatekelezwe na kuheshimiwa.