Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchina inakuwa kwa kasi na kwa ushawishi mkubwa:Ban

Uchina inakuwa kwa kasi na kwa ushawishi mkubwa:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amehitimisha ziara yake nchini Uchina hii leo kwa hotoba maalumu.

Akihutubia katika mkutano maalumu kuhusu viongozi wa siku za usoni, utawala bora na jamii ya amani na utulivu kwenye Central Party School mjini Beijing Ban amesema Uchina inakuwa kwa kasi, mabadiliko yake ni ya kutia matumaini, ushawishi wake duniani umeongezeka na nguvu zake ni za dhahiri.

Ban ameelezea matumaini yake kwamba kukua kwa uchini kutakuwa na manufaa kwa dunia, lakini ameonya kwamba kukua kwa uchini kunakuja na matarajio makubwa na majukumu makubwa duniani. Ameongeza kuwa uongozi wa Uchina utahitajika katika masuala muhimu kama mabadiliko ya hali ya hewa ,amani na usalama wa dunia, suala la Myanmar, Korea na malengo ya maendeleo ya milenia.

Amehitimisha hotuba yake kwa kuelezea kujiamini kwake kwamba kwa ushirikiano pamoja na Uchina na jumuiya nzima basi dunia itaelekea kwenye kuwa na utawala bora na maisha bora kwa wote.