Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fadhila japo kidogo yaweza kubadili maisha ya watu:Mburu

Fadhila japo kidogo yaweza kubadili maisha ya watu:Mburu

Je fadhila kidogo inaweza kubadili maisha? Mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa mataifa Chris Mburu anasema bila shaka.

Chris Mburu ni mwanasheria kwenye ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, alizaliwa na kukulia nchini Kenya katika hali ya umasikini mkubwa.Anasema anashukuru ufadhili aliopata kutoka kwa mwanamke mmoja wa Sweeden uliomsaidia kupata elimu ya sekondari hadi chuo kikuu cha Harvad.

Chris hakumfahamu huyo mwanamke lakini miaka 30 baadaye ameweza kumshukuru kwa msaada wake wa dola 15 kila muhula wa shule na akaweza kubadili maisha yake kabisaa. Leo hii Chris ameweza kuanzisha mfuko maalumu wa kuhakikisha watoto wengine wenye uwezi kiakili kutoka kijijini kwake wanapata elimu.

Historia hii ya Chris ipo kwenye filamu fupi iitwayo A Small Act iliyoshinda tuzo na imeaanza kuonyeshwa kwenye jumba la Cinema la Quad hapa New York. Amezungumza Flora Nducha na kumueleza imekuaje hata mambo yakafikia hapa.