Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhalifu Darfur unatia hofu asema mkuu wa usalama wa UM

Uhalifu Darfur unatia hofu asema mkuu wa usalama wa UM

Vitendo vya uchukuaji watu mateka kwenye jimbo la Darfur Sudan vimeendelea kuutia hofu Umoja wa Mataifa amesema mkuu wa idara ya usalama ya Umoja wa Mataifa.

Hivi sasa mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anashikiliwa na kundi la watu wasiojulikana kwenye jimbo la Darfur Akizungumza mjini El Fasher makao makuu ya mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na ule wa afrika UNAMID Gregory Starr amesema hali ya ulinzi na usalama kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Darfur ni ya lazima na muhimu.

Amesema kuna mfanyakazi wetu mmoja ambaye ni mateka kwa wakati huu kutokana na kile kinachoonekana kundi la kihalifu. Utekaji umekuwa tatizo hapa kwa siku za nyuma na kwa bahati mbaya bado unaendelea sasa.

Na haya ni masuala yanayotia hofu kubwa. Ulinzi na usalama na hali ya wafanyakazi wetu ni suala ambalo lazima tulichukulie kwa uzito mkubwa na tutajitahidi iwezekanavyo kumrudisha mateka hutyo.